Thursday, May 21, 2020

CHIEF MORISON AKUTANA NA MHE. HARRISON MWAKYEMBE

Tarehe 2 Julai, 2018 Jumatatu Chief Morison alikutana na Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe kwenye Wizara yake akiwa na lengo la kuzungumza nae masuala mbalimbali katika michezo ila kubwa lilikuwa ni kwenda kushiriki mchuano wa mchezo wa Freestyle Football nchini Nigeria katika Ubingwa wa Bara la Afrika.

MGAO WA VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI WADOGO RUVUMA

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, CHRISTINA Mndeme amegawa vitambulisho 9,000 vya wajasiriamali wadogo kwa wakuu wa wilaya zote ili kusambaza kwa wafanyabiashara hao.

Sunday, November 12, 2017

Morison Mosses Jumanne ndiye Mwenyekiti wa Klabu ya Wamachinga Tanzania.

Afisa Habari Mkuu alitoa taarifa kwa Umma na vyombo vya habari kwa niaba ya Mwenyekiti wa Klabu (WASPOC), Uongozi wa Klabu na Chama cha Wamachinga Kariakoo (KAWASSO)

Tuesday, December 6, 2016

Shindano la ubingwa wa Kuchezea mpira wa miguu Dar Es Salaam Freestyle Football Championship kutimua vumbi UBUNGO Jumamosi hii.

DFFC yaliyoandaliwa na FREESTYLE FOOTBALL TANZANIA na kudhaminiwa na Redbull Tanzania na kushirikiana na wabia mbalimbali yalisimama Jumamosi iliyopita ya tarehe 03 Disemba na kupangwa kuendelea tarehe 10 Disemba Jumamosi hii.

Taarifa zaidi wasiliana na Kurugenzi ya mawasiliano ya Freestyle Football Tanzania: 0786955825 / 0655049647 au tembelea Instagram: @freefoottanzania

Monday, November 7, 2016

UONGOZI WA UCHEZEAJI MPIRA WA MIGUU TFFA YAINGIA UBIA RASMI NA KAMPUNI YA SHAFFIH DAUDA, SHADAKA WASIMAMIZI WA MICHEZO

Leo tarehe 07 Novemba 2016, siku ya kufanyika shindano la kuchezea mpira wa miguu Duniani (WORLD FREESTYLE FOOTBALL CHAMPIONSHIP 2016) linalofanyika nchini Uingereza jiji la London usiku mpaka kesho 08 Novemba mwisho wa shindano hilo maarufu kama Redbull Street Style.
Huku kwetu Tanzania Serikali ya mchezo huo inayotawaliwa na klabu mama ya kuchezea mpira wa miguu Genius MP imeingia makubaliano na Kampuni ya usimamizi wa michezo Shadaka (Shadaka Sports Management) kwa muda wa miaka 5 kwa lengo la kuratibu matukio na mashindano yote ya FFT.

Tuesday, October 4, 2016

Freestyle Football Tanzania yajipanga kutangaza nafasi kwa washiriki (FOOTBALL FREESTYLERS)

Tumeamua rasmi kutangaza nafasi kwa washiriki yaani Football Freestylers nchini kwa kutuma maombi yao kwa kutuma video isiyozidi dakika 2 kwenye mitandao ya kijamii ambayo ipo katika posters tulizozitengeneza

Mawasiliano 👇
0786955825

Thursday, May 26, 2016

Klabu ya GENIUS MP Freestyle yaanza kwa Mhe. Jakaya M. Kikwete leo

Klabu mama ya Kuchezea mpira wa miguu Genius MP yaanza kusajili wachezeaji leo na imeanza rasmi kutumia viwanja vya Mhe. Rais mstaafu Jakaya M. Kikwete pale kidongo chekundu park. Tukizungumza na mmiliki wa Klabu ya Genius MP na mwanzilishi wa Vilabu na Vyama vya Freestyle Football Tanzania (FFT) Bw. Morison Mosses na Makamo wake Bw. Pascal Chang'a wamesema wamependezwa na muitikio wa wachezeaji kujitokeza sana na wamesema wachezeaji (Freestylers) wazidi kujitokeza sasa maana ni wakati wao. Kutana na #Ronaldinho sasa.
#SanaaYaSoka.BurudaniTosha