Hadhara Charles ni maarufu kwa kuchezea mpira wa miguu nchini Tanzania. Huwa anapatikana kwa kazi yake kwenye mechi kubwa kama Simba na Yanga, timu za taifa zinapocheza na kwenye hafla mbalimbali bila kusahau kwenye kampeni za uchaguzi 2015 alikuwa akifanya kazi yake.
Morison Blog ilipata taarifa kutoka kwa baba mdogo wa Hadhara Charles na kusema kuwa Hadhara amepata ajali ya kuunguzwa na maji ya moto sehemu kubwa wa mwili wake na shangazi yake. Kwsa sasa, mwanadada huyo amelazwa hospital ya Mwananyamala.