Mahojiano hayo yalikuwa mwenyekiti na mwanahabari:
Charles Abel Mwananchi: Ukiwa kama mwenyekiti wa chama cha kuchezea mpira wa miguu Tanzania, hotuba ya Waziri na tukio la yeye kukutana na viongozi wa vyama na mashirikisho ya michezo umeipokeaje?.
Morison Mosses TFFA: Nikiwa kama Mwenyekiti wa chama cha Kuchezea Mpira wa miguu Tanzania (Tanzania Freestyle Football Associatian) tukio la waziri kukutana nasi nimelipokea ni jambo nzuri sana:
1. Kwa utawala wa awamu ya 5 unatuonesha utakuwa pamoja nasi katika misingi imara ya kuimarisha michezo.
2. Kutuonesha mshikamano wa pamoja.
3. Kutuonesha msisitizo wa majukumu ya serikali (wizara ya michezo, baraza la michezo na ngazi zake) upande wa michezo utazingatiwa kwa bidii.
4. Kutuonesha kwamba baadhi ya vipengele vya sera na sheria ni kandamizi kwetu hivyo vitashughulikiwa kwa kufanyiwa mabadiliko.
Charles Abel Mwananchi: Kuna hoja ilitolewa juu ya katiba za vyama vingi nchini kutengenezwa kwa misingi ya kuwalinda viongozi wa vyama hivyo kukaa madarakani muda mrefu. Je nyie kwa upande wenu mnalionaje hilo?.
Morison Mosses TFFA: Ndio, ni kweli katiba za vyama vingi nchini kutengenezwa kwa misingi ya kuwalinda viongozi ila kwa upande wetu TFFA / CHAKUMMI tunaliona ni tofauti kutokana na makubaliana yaliyo ndani ya katiba yetu muda wa kukaa madarakani ni mchache sana kwa kuzingatia ni chama kipya. Lakini kwa upande wa vyama vipya vinatakiwa iwe hivyo viongozi wakae madarakani maana wengi wao ni waanzilishi lakini kwa vile vyama vya zamani wanatakiwa wafanye mabadiliko ya uongozi wa kukaa madarakani muda mrefu.
Charles Abel Mwananchi: Nashukuru sana kiongozi kwa ushirikiano wako.
Morison Mosses TFFA: Nashukuru pia na wewe kiongozi.