Saturday, August 25, 2012

MESSI PENALTY KING

Lionel Messi scored another goal from
the penalty spot as Barcelona
defeated rivals Real Madrid by three
goals to two in the first leg of the
Spanish Super Cup.

Van Persie strikes as ManUtd edge to win

Van Persie & Kagawa score as
hosts secure first win of
season.

Kikosi cha MAN United kilichoichapa Fulham

LINEUPS
1 De Gea
15 N. Vidić
3 P. Evra
2 Rafael
16 M. Carrick
7 A. Valencia
18 A. Young
8 Anderson
23 T.Cleverley
20 R. van Persie
26 S. Kagawa
Coach: A. Ferguson

TOMORROW:OSASUNA vs BARCELONA

OSASUNA
19:00
BARCELONA

Competition
Primera División

Date
26 August 2012

Game week
2

Kick-off
19:00

ADDITIONAL INFO
Referee César Muñiz Fernández

Assistants
Jose Manuel Fernandez Miranda
Enrique Andres Samper

Fourth official
Ignacio Hermosilla

MANCHESTER UNITED 3 VS 2 FULHAM

0 - 1 3' D. Duff (G) (assist by B. Ruiz)
R. van Persie (G)10' (assist by P. Evra)1 - 1
S. Kagawa (G)35' 2 - 1
Rafael (G)41' (assist by A. Young)3 - 1
3 - 2 64' N. Vidić (OG)

NEW VIDEO:I'm your leader_Nick Minaj ft. Cam'Ron & Rick Ross

Nice video

Sina Hali song_Muddy Classic

Artist:Muddy Classic
Song:Sina Hali
Producer:Minyo Masonge
Studio:Hisia Records

Tutapata Chorus Lyric-Suistar ft. Minyo

Chorus
Shida na karaha,vumilia dada
Nasi tutapata,maisha tutashinda
Shida na karaha,vumilia dada
Nasi tutapata,maisha tutashinda
Tusiogope kuchekwa aaah
Mungu ndiye aliyepanga aaah

Michael Jackson wa bongo na Suistar Mo Silver watakapokutana

Kipindi cha NigongeeTV cha DTV na Rick Ross wa bongo

The video making of Muddy Classic

Muddy classic

KESHO:Liverpool vs Manchester City

Hii ni mechi kali ambayo mashabiki wa timu zote mbili wanaisubiri kwa hamu.

Zambia ina lugha tisa(9) katika kuu tatu(3)

Zambia inatumia English,Nyanja,Bemba,Kaonda,Lozi,Lunda,Luvale,Tonga

I Still Love Zambia

Zambia ni nchi nzuri kama ilivyo Tanzania.

This Is Diamond

The Video making of Coca Cola Vuta
Mkwanja na Diamond Platnum ilivyokuwa.Get more news kwenye blog yake www.thisisdiamond.com.

KIMYA:BARCELONA ilivyowaliza mashabiki wa REAL MADRID

Mashabiki wa Real Madrid walipolizwa na Barcelona baada ya ushindi mnono wa 3-2 wa Barcelona

WAISLAMU ZAIDI WAKUBALI SENSA

IKIWA imebaki siku moja kabla ya Taifa kuingia katika Sensa ya Watu na Makazi, viongozi wa Jumuiya ya Kuendeleza Kuran na Suna Tanzania (JUQUSUTA) wamesema kuwa Waislamu nchini wako tayari kushiriki. Viongozi hao wakiwemo Mashehe, Maimamu na waumini wa dini ya Kiislamu walio chini ya Juqusuta, waliyasema hayo jana wakati walipokuwa wakitoa tamko lao la kushiriki kwenye Sensa baada ya kuhitimisha mkutano wao wa siku mbili uliofanyika jijini hapa, uliozungumzia mambo mbalimbali yahusuyo mustakabali wa jumuiya yao. Awali Mwenyekiti wa Juqusuta, Shehe Hassan Kabeke alisema kuwa azimio hilo limefikiwa na viongozi hao wa kitaifa baada ya kuchoshwa na propaganda zinazoenezwa na kikundi cha watu wachache wakiwataka waislamu wasishiriki kwenye sensa, na kusema kuwa nia ya watu hao ni kuwagombanisha Waislamu na Serikali iliyoko madarakani. Alisema watu wanaosambaza vipeperushi vya uchochezi wana sababu zao binafsi na kwamba wamekuwa wakifanya hivyo kuutafuta umaarufu kupitia Sensa na kwamba Uislamu au dini ya Kiislamu haikatazi watu au waumini wao kuhesabiwa. “Uislamu haukatazi Sensa isipokuwa kuna watu aidha kwa manufaa yao binafsi, kwa kutafuta umaarufu wanawakataza baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wasishiriki Sensa, ila sio kwa manufaa ya Uislamu bali ni kwa manufaa yao wenyewe. “Mwongozo wa Uislamu ni Kuran, hakuna mahali kwenye Kuran au katika hadithi za Mtume Muhammad panapokataza waumini wa dini ya kiislamu wasihesabiwe, Mtume Muhammed mwenyewe alifanya Sensa kujua idadi ya Waislamu wa Madina na Macca, hawa wanaohamasisha waumini kutoshiriki katika Sensa wanapata wapi Sheria hiyo endapo Mtume Muhammad yeye alishiriki katika kuhesabu watu?” alihoji. Kabeke alitumia fursa hiyo kuiomba Serikali kuwaachia huru waumini wa dini ya Kiislamu waliotiwa mahabusu na wanaoendelea kukamatwa na jeshi la polisi, wakisema walipotoshwa bila kujua ukweli ukoje, na badala yake wakamatwe wanaochochea kampeni chafu dhidi ya Sensa. Aliwataka Waislamu nchini kote kutokubali kampeni au uhamasishaji wa aina yoyote wenye lengo la kuwataka kutoshiriki katika Sensa na kuwataka watambue kuwa kwa muislamu anayegoma kushiriki katika Sensa au kushawishi watu wasishiriki katika Sensa atakuwa ameingia kwenye dhuluma. “Tunalaani taasisi nyingine za Kiislamu zinazowashawishi waumini kutoshiriki Sensa maana kwa kufanya hivyo ni kukiuka maadili ya Dini ya Kiislamu, na baadhi ya vyombo vya habari vinavyoeneza propaganda hizo ni vyema vikaacha maana vinaupotosha umma na waumini wa dini ya Kiislamu”, aliongeza Naye Makamu Mwenyekiti wa Juqusuta, Shehe Mohamedi Said alisema kuwa kuhusu kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi, wameridhia uteuzi uliofanywa na Mufti wa Tanzania, Issa Shaaban bin Simba katika uteuzi wa Kadhi Mkuu Shehe Abdallah Myasi na kwamba uteuzi wake ni sahihi na wanauunga mkono. Katika tamko la pili lililotolewa na Juqusuta, aliwataka waislamu kutambua kuwa Sensa ni halali kwa mujibu wa Sheria na aliwataka waislamu wote nchini kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa makarani wa Sensa ili waweze kufanikisha zoezi hilo. Kwa upande wake Mlezi wa Jamii ya Kiislamu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAMCO), Altaf Hirani ambaye alifunga mkutano huo, aliwataka Waislamu nchini kufuata maadili ya Kiislamu na wasifanye mambo yao kwa kutumia jazba, bali jazba wazitumie katika misikiti na sio kuonesha jazba hizo mbele ya jamii. Jeshi la Polisi laonya Wakati Waislamu wakihimizana kushiriki katika Sensa, Jeshi la Polisi nchini limewaonya wanaoshawishi watu kugomea huku wakitaka waripotiwe mara moja ili wakamatwe kwa kuwa watakuwa wanavunja sheria za nchi. Pamoja na kutoa onyo hilo, jeshi hilo limeutaka umma kutohofia hali ya ulinzi na usalama wakati wa ushiriki wa operesheni hiyo kwa vile limejipanga kuhakikisha kunakuwa na usalama. Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba alisema jeshi linafahamu kuhusu uwepo wa watu wachache wanaoendelea kukataza wengine wasishiriki kuhesabiwa kwa kuwapa vitisho mbalimbali, kinyume cha sheria. “Sensa ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania sasa wanapotokea wachache na kuwachochea wengine wasiishiriki inakuwa ni kuvunja sheria. Nawaomba Watanzania waendelee kutujuza kuhusu wanaowakataza wasikubali kuhesabiwa ili tuwachukulie hatua zinazostahili kwa sababu wanachokifanya ni uhalifu,” Manumba alisema. Alieleza kuwa tayari jeshi hilo limekwisha wachukulia hatua mbalimbali wachochezi waliokamatwa katika mikoa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani. “Jitokezeni kuhesabiwa bila hofu ya kuadhibiwa na wanaowakataza kwa sababu jeshi lenu lipo na limejipanga vuizuri kudhibiti hali hiyo. Wanaowafuata nyumbani, ofisini na katika maeneo mengine mliyopo ili kuwashawishi msihesabiwe wanawanyima haki yenu ya msingi, hivyo tuleteeni taarifa zao tuwashughulikie kwa mujibu wa sheria,” aliongeza. Kwa upande wake, Kamishna wa Operesheni Maalumu na Mafunzo katika jeshi hilo, Paul Chagonja alisema
kitendo cha kikundi au taasisi kuwakataza watu wake wasishiriki sensa hakivumiliki kwa sababu kina lenga kukwamisha maendeleo ya nchi bila sababu za msingi.

Misa Ya Wafu Yafanyika AFRIKA KUSINI

Maelfu ya watu nchini Afrika Kusini
wamehudhuria misa ya kuwaombea
watu waliouawa katika machimbo ya
Marikana ya madini ya Platinum. Watu thelathini na wanne waliuawa na
polisi kwa kupigwa risasi wakati wa
maandamano ya wachimba mgodi huo
wakidai malipo zaidi, wiki moja iliyopita. Misa hiyo ilivurugwa kwa muda
kufuatia kuwasili kwa mamia ya
wafanyakazi wa mgodi walio katika
mgomo, baadhi yao wakiwa wamebeba
mapanga. Misa kama hiyo zinafanyika nchini
kote Afrika Kusini. Rais Jacob Zuma anatarajiwa kuanisha
hadidu za rejea kwa tume ya
kuchunguza mauaji hayo. Bwana Zuma hakushangiliwa wakati
alipotembelea eneo la tukio la mgodi
wa Marikana Jumatano. Mgogoro huo umesambaa katika
migodi mingine ya platinum nchini
humo. Afrika Kusini inazalisha robo tatu ya
madini hayo ya Platinum kote duniani
na bei ya madini hayo imepanda
kutokana na wasiwasi wa kushuka
kwa uzalishaji nchini Afrika Kusini.

LIGI KUU UINGEREZA HII LEO:Tabiri nasi

Chelsea vs Newcastle
Man U vs Fulham

SENSA 2012:Sensa kwa maendeleo,jiandae kuhesabiwa,kuanzia kesho tarehe 26 Agosti 2012

Ni muhimu kwa kila mtu kuhesabiwa

Suistar Mo Silver ft Minyo_Tutapata

New song ya Suistar akiwa amemshirikisha Minyo ambaye ni producer wa studio ya Hisia Records.

Martin kadinda Official Fashion Blog: SAFIIIIIIIIIIIIIIIIIII: OMMY DIMPOZI & DIAMOND PLATNUMZ

Martin kadinda Official Fashion Blog: SAFIIIIIIIIIIIIIIIIIII: OMMY DIMPOZI & DIAMOND PLATNUMZ

When I was in Zambia

I'm Suistar