Thursday, March 21, 2013

TRA MKOA WA KODI ILALA LAWAKUMBUSHA WAFANYABIASHARA WOTE KUJAZA NA KULETA RITANI YA MAKADIRIO YA KODI NA KULIPA AWAMU YA KWANZA.

Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kodi Ilala inawakumbusha wafanyabiashara wote kuwa tarehe ya mwisho ya kujaza ritani ya makadirio ya kodi na kulipa awamu ya kwanza ya kodi ya mapato kwa mwaka 2013 ni tarehe 31 Machi 2013. Kwa wale wenye malimbikizo ya kodi ya vipindi vya nyuma wanakumbushwa kulipa kabla ya tarehe 31 Machi 2013.

Baada ya tarehe hiyo msako mkali utafanyika kufuatilia wote ambao hawajaleta ritani za makadirio kwa kipindi hiki. Adhabu itatolewa kwa mujibu wa kifungu namba 98 cha sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004.

Wahi sasa kuepuka usumbufu.

“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”.