Friday, August 28, 2015

WhatsApp ya Android yapata 'Update' fahamu mambo 5 yaliyoboreshwa

Baada ya muda mrefu wa majaribio, yaani beta,
toleo jipya la WhatsApp kwa ajili ya Android laja
likiwa na sifa 5 kubwa za maboresho mazuri zaidi kama zifuatazo:
1. Soma halafu fanya ujumbe husika kama haujasomeka, yaani 'Mark as unread'.

2. Milio spesheli kwa watu mbalimbali.

3. Nyamazisha miito kwa mtu mmoja mmoja (mute).

4. Tumia kiasi kidogo cha data pale unapopiga simu za whatsapp.

5. Emoji mpya na chaguo la rangi zake.

Baadhi ya shule DSM zimefungwa kunusuru wanafunzi na maambukizo ya ugonjwa wa Kipindupindu

Baadhi ya shule jijini Dar es Salaam zimefungwa kunusuru wanafunzi na maambukizo ya ugonjwa wa kipindupindu na kuwanusuru wanafunzi kupata ugonjwa huo ambao kwa sasa umeonyesha dhahiri kuwa bado ni tishio kutokana idadi ya watu wapya kuendelea kubainika kuwa na ugonjwa huo kila siku katika manispaa zote tatu za jiji licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na manispaa hizo.
 
ITV imetembelea baadhi ya shule na kuzungumza na walimu na wanafunzi ambapo kaimu makamu mkuu wa shule ya sekondari ya White Lake mwalimu Abel Elias amesema wamelazimkka kufunga shule kwa kipindi cha wiki mbili ili kuupisha ugonjwa huo kupita bila ya kuleta athari kwa wanafunzi.
 
Aidha kituo hiki kimetembealaea kambi za kipindu pindu ambapo katika kambi manispa ya Ilala kuna wagonjwa wapya 15 na jumla ya watu 63 tayari wanapatiwa matibabu ya ugonjwa huo.
 
Kwa upande wa manispa ya Kinondoni bado hali ni mbaya kwa sababu wagonjwa wapya wameendelea kufikishwa katika kambi ya Mburahati  na katika manispa ya Temeke kuna wagonjwa wanne waliolazwa katika kambi iliyopo katika hospitali ya Temeke.
 
Naye msimamizi wa kituo ch afya Buguruni ambapo ndipo ngome ya wagonjwa wa kipindupindu ilipo amesema tatizo kubwa jamii bado haijauchukulia ugonjwa huu kama ni tatizo kubwa na kama watu hawatabadili tabia ni wazi kuwa tatizo litazidi kuwa kubwa.

WAMEBANA WAMEACHIA, LOWASA AUNGURUMA KESHO JANGWANI

Mgombea kiti cha uraisi wa CHADEMA Mhe. Edward LOWASA atahorubia kesho jangwani katika uzinduzi rasmi wa kampeni.