Baadhi ya shule jijini Dar es Salaam zimefungwa kunusuru wanafunzi na maambukizo ya ugonjwa wa kipindupindu na kuwanusuru wanafunzi kupata ugonjwa huo ambao kwa sasa umeonyesha dhahiri kuwa bado ni tishio kutokana idadi ya watu wapya kuendelea kubainika kuwa na ugonjwa huo kila siku katika manispaa zote tatu za jiji licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na manispaa hizo.
ITV imetembelea baadhi ya shule na kuzungumza na walimu na wanafunzi ambapo kaimu makamu mkuu wa shule ya sekondari ya White Lake mwalimu Abel Elias amesema wamelazimkka kufunga shule kwa kipindi cha wiki mbili ili kuupisha ugonjwa huo kupita bila ya kuleta athari kwa wanafunzi.
Aidha kituo hiki kimetembealaea kambi za kipindu pindu ambapo katika kambi manispa ya Ilala kuna wagonjwa wapya 15 na jumla ya watu 63 tayari wanapatiwa matibabu ya ugonjwa huo.
Kwa upande wa manispa ya Kinondoni bado hali ni mbaya kwa sababu wagonjwa wapya wameendelea kufikishwa katika kambi ya Mburahati na katika manispa ya Temeke kuna wagonjwa wanne waliolazwa katika kambi iliyopo katika hospitali ya Temeke.
Naye msimamizi wa kituo ch afya Buguruni ambapo ndipo ngome ya wagonjwa wa kipindupindu ilipo amesema tatizo kubwa jamii bado haijauchukulia ugonjwa huu kama ni tatizo kubwa na kama watu hawatabadili tabia ni wazi kuwa tatizo litazidi kuwa kubwa.
Friday, August 28, 2015
Baadhi ya shule DSM zimefungwa kunusuru wanafunzi na maambukizo ya ugonjwa wa Kipindupindu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment