Tuesday, August 28, 2012

Hali ya hatari katika jimbo la Louisiana

Rais barack Obama ametangaza hali
ya hatari katika jimbo la Louisiana
nchini Marekani linalotishiwa na
kimbunga Isaac. Kimbunga hicho
kinatarajiwa kufika ardhini jioni ya leo
ikiwa miaka saba tangu kutokea gharika la Katrina katika eneo la New
Orleans. Kwa sasa kimbunga Isaac kimetajwa
kuwa bado ni tufani japo kinatarajiwa
kushika kasi zaidi na kuwa kimbunga
kamili la uharibifu mkubwa inapoelekea
kuvuka ghuba ya Mexico. Kimbunga kama hicho kwa jina
Katrina, kiliwaua zaidi ya watu elfu
moja mia nane mjini New Orleans
mnamo agosti mwaka wa elfu mbili na
tano. Tangazo hilo la hali ya hatari
litawezesha afisi za serikali kutenga
fedha za kutosha kwa ajili ya misaada
baada ya kimbunga kupita. Kimbunga hicho kinapiga miaka saba
baada ya kimbunga kibaya zaidi
kuwahi kushuhudiwa nchini Marekani
cha Katrina kugonga Marekani. Chama cha Republican kimelazimika
kuchelewesha kongamano lake la
kitaifa , mjini Tampa, Florida
kumchagua rasmi mgombea wa urais
kwa chama hicho atakayepambana na
rais Barack Obama. Kimbunga saac kiliwaua watu 24 nchini
Haiti na katika Jamuhuri ya Dominica
na pia kusababisha uharibifu mkubwa
katika visiwa vya Caribbea. Hapo jana, kituo cha kitaifa cha
kutabiri vimbunga, kilionya kuwa
huenda kimbunga hicho kikafikia
daraja ya pili kikiambatana na
mawimbi makali yenye kasi ya kilomita
160, kwa saa. Rais Obama aliitikia wito wa jimbo la
Louisiana kuitaja hali kuwa ya hatari,
na kuwezesha jimbo hilo kupokea
msaada wa kitaifa kupambana na hali.

Wanawake Togo wasusia ngono kudaiMageuzi

Wanawake nchini Togo, wametakiwa
kususia kitendo cha ndoa kuanzia
Jumatatu wiki hii kama njia ya
kushinikiza serikali kuleta mageuzi. Kampeini hiyo yenye kauli mbiu ''Juhudi
za kuokoa Togo'' imeanzishwa kwa
ushirikiano na mashirika tisa ya kijamii
pamoja na vyama saba vya upinzani
pamoja na vyama vingine vya kijamii. Kiongozi wa upinzani, Isabelle
Ameganvi alisema kuwa kususia ngono
huenda ndio itakuwa silaha inayofaa
kuweza kuleta mageuzi ya kisiasa. Muungano wa vyama hivyo pamoja na
mashirika yasiyo ya kijamii unataka
rais Faure Gnassingbe, ambaye familia
yake imeshikilia madaraka kwa miaka
mingi waweze kuondoka mamlakani. "tuna njia nyingi za kuwashinikiza
wanaume kuelewa tunachotaka sisi
wanawake'' alisema bi Ameganvi,
kiongozi wa tawi la wanawake la
muungano huo. Alisema kuwa yeye ameweza
kushawishiwa na mgomo sawa na huo
nchini Liberia mwaka 2003,ambao
walitumia njia ya kususia ngono
kushinikiza amani. "ikiwa wanaume watakataa kusikia
kilio chetu, tutalazimika kufanya
maandamano ambayo yatakuwa makali
zaidi kuliko mbinu hii ya kususia
ngono.'' aliongeza bi Ameganvi Togo imekuwa ikiongozwa na familia
moja kwa zaidi ya miaka arobaini. Rais President Faure Gnassingbe
alichukua mamlaka mnamo mwaka
2005 kufuatia kifo cha babake
Gnassingbe Eyadema, aliyetawala Togo
kwa miaka 38. Rais alichaguliwa kwa
muhula mwingine mnamo mwaka 2010. Mgomo huo ulitangazwa katika
mkutano wa hadhara mnamo siku ya
Jumamosi mjini Lome, na ambao
ulihudhuriwa na maelfu ya watu. Mkutano huo ulifanyika kupinga
mabadiliko ya hivi karibuni
yaliyofanywa ambayo wakereketwa
wanasema kuwa yatarahisisha ushindi
wa chama tawala cha Gnassingbe
kuweza kwenye uchaguzi wa bunge utakaofanyika mwezi Oktoba. Wanaharakati wanasema kuwa mgomo
huo utashinikiza wanaume ambao
hawajihusishi na mchakato wa kisiasa
kuweza kuhakikisha malengo yake
yanatimizwa ambayo ni pamoja na
kukomeshwa kwa utawala wa rais usio na kikomo. Mapema mwezi huu, waandamanaji
wanaopinga utawala wa rais
Gnassingbe walitawanywa na polisi
kwa kutumia gesi ya kutoa machozi
na wengine zaidi ya miamoja
wakakamatwa.

ZOEZI LA SENSA-KAGERA

Watu 11 watiwa mbaloni na polisi baada ya kuhamasisha sensa.

DON`T MISS OUT TO WATCH THE MISS EAST-AFRICA COMPETITION ''LIVE'' ON M-NET www.whoissuistar.blogspot.com

Mashindano ya Miss East Africa
mwaka huu yataonyeshwa LIVE
kupitia Mnet ambapo yanatarajiwa
kutuizamwa na watu wanaokadiliwa
kufikia million 200 kupitia televison
na kwa njia ya internet Dunia nzima. Aidha maandalizi ya mashindano
hayo yanaendelea kwa kasi ambapo
yamepangwa kufanyika tarehe 07
December, 2012 katika ukumbi wa
Mlimani City, jijini Dare s salaam,
Tanzania badala ya mwezi September kama ilivyokuwa
imetangazwa awali ili kutoa muda
zaidi kwa Ncgi ambazo hazijapata
wawakilishi wao kuweza kukamilisha
zoezi hilo. Mashindano ya Miss East Africa
mwaka huu yanatarajiwa kuwa na
mvuto wa aina yake ambapo
yatashirikisha warembo kutoka
katika Nchi 16 za ukanda wa afrika
mashariki. Nchi zilizothibitisha kushiriki
mashindano hayo ni wenyeji
Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda
na Burundi. Nchi zingine zilizoalikwa
kushiriki ni pamoja na Ethiopia,
Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan, Malawi, pamoja na visiwa vya
Seychelles, Madagascar, Reunion,
Comoros, na Mauritius. Mashindano ya Miss East Africa
yanalenga kukuza ushirikiano na
kutangaza utamaduni wa Afrika
mashariki, pamoja na kutangaza
utalii wa Tanzania kama Nchi wenyeji
wa mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa Afrika Tayari baadhi ya Nchi zinazoshiriki
mashindano hayo zimeshatangaza
wawakilishi wake ambazo ni Eritrea,
Ethiopia, Uganda, Southern Sudan,
Malawi na Seychelles. Nchi zilizosalia
zinatarajiwa kutangaza wawakilishi wao kabla ya tarehe ya mwisho
ambayo ni tarehe 28 mwezi
September. Mashindano ya Miss East Africa
yanamilikiwa na kuandaliwa na
kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini
Dar es salaam,

MTU MMOJA AKAMATWA NA POLISI ZNZ

Kwa kosa kuamasisha watu wasishiriki sensa.