Rais barack Obama ametangaza hali
ya hatari katika jimbo la Louisiana
nchini Marekani linalotishiwa na
kimbunga Isaac. Kimbunga hicho
kinatarajiwa kufika ardhini jioni ya leo
ikiwa miaka saba tangu kutokea gharika la Katrina katika eneo la New
Orleans. Kwa sasa kimbunga Isaac kimetajwa
kuwa bado ni tufani japo kinatarajiwa
kushika kasi zaidi na kuwa kimbunga
kamili la uharibifu mkubwa inapoelekea
kuvuka ghuba ya Mexico. Kimbunga kama hicho kwa jina
Katrina, kiliwaua zaidi ya watu elfu
moja mia nane mjini New Orleans
mnamo agosti mwaka wa elfu mbili na
tano. Tangazo hilo la hali ya hatari
litawezesha afisi za serikali kutenga
fedha za kutosha kwa ajili ya misaada
baada ya kimbunga kupita. Kimbunga hicho kinapiga miaka saba
baada ya kimbunga kibaya zaidi
kuwahi kushuhudiwa nchini Marekani
cha Katrina kugonga Marekani. Chama cha Republican kimelazimika
kuchelewesha kongamano lake la
kitaifa , mjini Tampa, Florida
kumchagua rasmi mgombea wa urais
kwa chama hicho atakayepambana na
rais Barack Obama. Kimbunga saac kiliwaua watu 24 nchini
Haiti na katika Jamuhuri ya Dominica
na pia kusababisha uharibifu mkubwa
katika visiwa vya Caribbea. Hapo jana, kituo cha kitaifa cha
kutabiri vimbunga, kilionya kuwa
huenda kimbunga hicho kikafikia
daraja ya pili kikiambatana na
mawimbi makali yenye kasi ya kilomita
160, kwa saa. Rais Obama aliitikia wito wa jimbo la
Louisiana kuitaja hali kuwa ya hatari,
na kuwezesha jimbo hilo kupokea
msaada wa kitaifa kupambana na hali.
No comments:
Post a Comment