Wanawake nchini Togo, wametakiwa
kususia kitendo cha ndoa kuanzia
Jumatatu wiki hii kama njia ya
kushinikiza serikali kuleta mageuzi. Kampeini hiyo yenye kauli mbiu ''Juhudi
za kuokoa Togo'' imeanzishwa kwa
ushirikiano na mashirika tisa ya kijamii
pamoja na vyama saba vya upinzani
pamoja na vyama vingine vya kijamii. Kiongozi wa upinzani, Isabelle
Ameganvi alisema kuwa kususia ngono
huenda ndio itakuwa silaha inayofaa
kuweza kuleta mageuzi ya kisiasa. Muungano wa vyama hivyo pamoja na
mashirika yasiyo ya kijamii unataka
rais Faure Gnassingbe, ambaye familia
yake imeshikilia madaraka kwa miaka
mingi waweze kuondoka mamlakani. "tuna njia nyingi za kuwashinikiza
wanaume kuelewa tunachotaka sisi
wanawake'' alisema bi Ameganvi,
kiongozi wa tawi la wanawake la
muungano huo. Alisema kuwa yeye ameweza
kushawishiwa na mgomo sawa na huo
nchini Liberia mwaka 2003,ambao
walitumia njia ya kususia ngono
kushinikiza amani. "ikiwa wanaume watakataa kusikia
kilio chetu, tutalazimika kufanya
maandamano ambayo yatakuwa makali
zaidi kuliko mbinu hii ya kususia
ngono.'' aliongeza bi Ameganvi Togo imekuwa ikiongozwa na familia
moja kwa zaidi ya miaka arobaini. Rais President Faure Gnassingbe
alichukua mamlaka mnamo mwaka
2005 kufuatia kifo cha babake
Gnassingbe Eyadema, aliyetawala Togo
kwa miaka 38. Rais alichaguliwa kwa
muhula mwingine mnamo mwaka 2010. Mgomo huo ulitangazwa katika
mkutano wa hadhara mnamo siku ya
Jumamosi mjini Lome, na ambao
ulihudhuriwa na maelfu ya watu. Mkutano huo ulifanyika kupinga
mabadiliko ya hivi karibuni
yaliyofanywa ambayo wakereketwa
wanasema kuwa yatarahisisha ushindi
wa chama tawala cha Gnassingbe
kuweza kwenye uchaguzi wa bunge utakaofanyika mwezi Oktoba. Wanaharakati wanasema kuwa mgomo
huo utashinikiza wanaume ambao
hawajihusishi na mchakato wa kisiasa
kuweza kuhakikisha malengo yake
yanatimizwa ambayo ni pamoja na
kukomeshwa kwa utawala wa rais usio na kikomo. Mapema mwezi huu, waandamanaji
wanaopinga utawala wa rais
Gnassingbe walitawanywa na polisi
kwa kutumia gesi ya kutoa machozi
na wengine zaidi ya miamoja
wakakamatwa.
No comments:
Post a Comment