Maelfu ya watu nchini Afrika Kusini
wamehudhuria misa ya kuwaombea
watu waliouawa katika machimbo ya
Marikana ya madini ya Platinum. Watu thelathini na wanne waliuawa na
polisi kwa kupigwa risasi wakati wa
maandamano ya wachimba mgodi huo
wakidai malipo zaidi, wiki moja iliyopita. Misa hiyo ilivurugwa kwa muda
kufuatia kuwasili kwa mamia ya
wafanyakazi wa mgodi walio katika
mgomo, baadhi yao wakiwa wamebeba
mapanga. Misa kama hiyo zinafanyika nchini
kote Afrika Kusini. Rais Jacob Zuma anatarajiwa kuanisha
hadidu za rejea kwa tume ya
kuchunguza mauaji hayo. Bwana Zuma hakushangiliwa wakati
alipotembelea eneo la tukio la mgodi
wa Marikana Jumatano. Mgogoro huo umesambaa katika
migodi mingine ya platinum nchini
humo. Afrika Kusini inazalisha robo tatu ya
madini hayo ya Platinum kote duniani
na bei ya madini hayo imepanda
kutokana na wasiwasi wa kushuka
kwa uzalishaji nchini Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment