Saturday, July 11, 2015

Biashara 5 Unazoweza Kuanza Kufanya Bila Ya Kuwa Na Mtaji.

Kikwazo kikubwa cha watu wengi kuingia kwenye
biashara kimekuwa ni mtaji. Japo sio kweli
kwamba mtaji pekee ndio kikwazo, lakini wengi
wanaamini mtaji tu ndio unawazuia.
Lakini pia wakati huo ambao mtu hana mtaji
hakuna juhudi kubwa anazofanya ili kuhakikisha
anapata mtaji huo.
Sasa kufupisha habari leo JIONGEZE na biashara
hizi tano unazoweza kuanza kuzifanya bila ya
kuanza na mtaji wa fedha.
1. Biashara ya mtandao(Network marketing).
Hii ni biashara ambayo ni mkombozi kwa mtu
yeyote ambaye ana kiu ya kufikia mafaniki. Hapa
tanzania kuna makampuni mengi yanayofanya
biashara hii kamA Forever living, Oriflame, GNLD,
na mengineyo. Katika makampuni haya kuna
ambayo unaweza kuanza na kiasi cha chini sana
ambacho ni sawa na bure.
2. Biashara ya ushauri.
Je kuna kitu ambacho una utaalamu nacho? Je
kuna kitu ambacho unapenda sana kukifuatilia na
hivyo unakijua sana? Vizuri, kuna mtu anataka
kukijua ila hajui aanzie wapi. Kwa wewe kutoa ujuzi
na uzoefu wako unaweza kulipwa fedha.
3. Biashara ya taarifa(internet marketing).
Hii ni biashara ya kutoa taarifa kwa kupitia
mtandao wa intanet. Unaweza kuwa na blog yako
ambayo ni bure kuiendesha na baadae ukaanza
kupata kipato kizuri kupitia mtandao.
Soma; jinsi ya kutengeneza fedha kwa kutumia
mtandao wa intaneti.
4. Biashara ya uwakala wa mauzo(salesman.)
Kuna makampuni mbalimbali ambayo yanatumia
mawakala kuuza bidhaa au huduma zao. Kwa
wewe kujifunza na kuwa wakala wao unaweza
kupata kipato kizuri kwa njia ya kamisheni.
5. Biashara ya udalali.
Hii ni biashara ambayo wewe unamsaidia mtu
kupata kitu anachotaka na hana muda au uzoefu
wa kukipata. Kama ukiweza kuifanya biashara hii
kwa mbinu nzuri unaweza kutengeneza kipato
kizuri.
Angalizo; Biashara hizi zinahitaji wewe ufanye kazi
kwa bidii na maarifa na pia unaweza usione faida
mapema. Ila ukiweka malengo na mipango mizuri
utaona mafanikio makubwa baadae.
Uzuri ni kwamba unaweza kuanza biashara hizi
ukiwa bado umeajiriwa au upo masomoni.

No comments:

Post a Comment