Chama tawala nchini Tanzania Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kimemtangaza daktari John
Magufuli kuwa mgombea wake wa kiti cha Urais
katika uchaguzi mkuu wa ujao.
Daktari John Magufuli, alisajili asilimia 87 % ya kura
za wajumbe, hiyo ikiwa ni kura 2104.
Bi Amina Salulm Ali alimaliza katika nafasi ya pili
akiwa na asilimia 10.5 % ya kura zote ikiwa ni sawa
na kura 253.
Dk. Asha-Rose Migiro akijizolea asimilia tatu ya
kura ya wajumbe ama kura 59.
Kufuatia ushindi huo Daktari Magufuli ndiye atakaye
kuwa mgombea urais wa chama hicho katika
uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba
mwaka huu
Mpaka sasa haijafahamika nani atakuwa mgombea
mwenza.
Hata hivyo tetesi zilizoenea zinaashiria kuwa Amina
Salum Ali ana nafasi kubwa ya kuchaguliwa kuwa
mgombea mwenza kutokana na kwamba yeye ndio
amekuwa wa pili katika kinyang'anyiro hicho.
Pia ikizingatiwa kwamba yeye ni mtanzania
mwenye asili ya Zanzibar.
Sunday, July 12, 2015
MGOMBEA URAISI CCM NI JOHN MAGUFULI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment