Ndege ya INDONESIA yatoweka na abiria 54.
Mamlaka nchini Indonessia inasema kuwa ndege
moja ya abiria iliowabeba watu 54 wakiwemo
watoto watano imepoteza mawasiliano na idara ya
kituo cha udhibiti safari za ndege.
Maafisa wa idara ya uchukuzi wanasema kuwa
ndege hiyo inayomilikiwa na huduma ya Trigana Air
ililikuwa ikielekea katika mji wa Oksibil
mashambani,mashariki mwa jimbo la Papua kabla
ya kutoweka.
Msemaji wa wizara hiyo amesema kuwa hatua za
kuisaka ndege hiyo zimeanza na zinashirikisha
mamlaka ya eneo hilo na kwamba hali mbaya ya
hewa katika milima ya eneo hilo inaathiri harakati
hizo.
Waandishi wanasema kuwa taifa la Indonesia lina
rekodi mbaya ya ajali za ndege huku ajali mbili
zikiwa tayari zimeripotiwa mwaka mmoja ulioipita.
Ndege ya Indonesia Air ilianguka katika bahari ya
Java mwezi Disemba ilipokuwa ikitoka Sura Baya
kuelekea Singapore na hivyobasi kuwaua watu wote
192 walioabiri chombo hicho.
Vilevile ndege moja ya kijeshi ilianguka katika
makaazi ya watu huko Medan Sumatra mnamo
mwezi Julai na kuwaua zaidi ya watu 140.
No comments:
Post a Comment