Monday, August 27, 2012

Apple ilivyoipiku Samsung mahakamani

Jopo la mahakama moja ya Marekani
limeamua kuwa kampuni kubwa ya
teknolojia ya Korea Kusini, Samsung,
iliiga baadhi ya ufundi mpya wa
kampuni ya Marekani ya Apple kuunda
simu zake wenyewe za kisasa za smartphone na kumputa ndogo -
tablet. Baada ya kesi iliyoendelea kwa mwaka
mzima, ambayo ilichunguza mashtaka
kama 700 ya aina ya ufundi ulioigwa,
mahakama ya California yaliiamrisha
Samsung iilipe Apple fidia ya dola zaidi
ya bilioni moja. Samsung imelalamika kuwa Apple
inajaribu kuhodhi soko zima la
smartphone, na imesema itakata
rufaa. Zaidi ya nusu ya simu za smartphone
zinazouzwa duniani ni ama za Apple
au Samsung, na kampuni hizo mbili
zinashtakiana katika mahakama ya
nchi mbali mbali duniani.

No comments:

Post a Comment