Monday, August 27, 2012

Mwana anga mkongwe wa Marekani afariki

Rais Obama ameongoza katika sifa na
rambi-rambi zilizotolewa baada ya kifo
cha Neil Armstrong, mwana anga wa
kwanza kutua kwenye mwezi, ambaye
amefariki akiwa na umri wa miaka 82
kutokana na matatizo aliyopata baada ya upasuaji aliofanyiwa kwenye
moyo. Rais Obama alimuelezea Neil Armstrong
kwamba ni mmoja kati ya mashujaa
wakubwa wa Marekani, siyo wakati
wake tu, lakini katika historia ya nchi
hiyo piya. Mwenzake Armstrong katika safari ya
kihistoria ya kwenda mwezini mwaka
wa 1969 alikuwa Buzz Aldrin, ambaye
alisema Armstrong alikuwa rubani na
kamanda mahiri. Familia ya Neil Armstrong imetoa wito
kwa Wamarekani kuonesha heshima
zao kwa kufuata mfano wake wa
kutumika, kufanikiwa na bila ya
majivuno. Taarifa ya familia iliwaambia wale
washabiki wake: "ukitembea nje usiku
ukaona mwezi unakuchekea, mfikirie
Neil na umkonyeze."

No comments:

Post a Comment