Tuesday, July 7, 2015

Mtandao usiokubali dhambi wavutia wengi

Waanzilishi wa Facegloria wanadai kwamba
mtandao huo umewavutia wafuasi takriban laki
moja tangu uzinduliwe mwezi Juni.
Kuna maneno 600 yaliopigwa marufuku katika
mtandao huo na kuna kibonyezo cha "Amen"
kushabikia ujumbe unaobandikwa.
Ummaland, ni mtandao wa kijamii wa kiislamu
uliozinduliwa 2013, can una wafuasi 329,000.
Unatoa fursa kwa wanawake kuwa na faragha zaidi
na kutoa ujumbe wa nasaha wa kidini kila siku.
Facegloria nchini Brazil kwa sasa unapatikana kwa
lugha ya kireno lakini waanzilishi wanataka
kuigeuza kwa lugha nyingine pia.
"Kwenye Facebook unashuhudia uchafu mwingi na
ghasia, ndio sababu tulifikiria kuanzisha mtandao
ambao utaturuhusu kuzungumza kuhusu Mungu
upendo na kusambaza neno lake," mtengenezaji
mtandao Atilla Barros ameiambia AFP.
Pia ni marufuku kubandika chochote
kinachohusiana na mapenzi ya jinsia moja.
Barros na waanzilishi wenzake watatu walikuwa
wakihudumu katika ofisi ya Acir dos Santos, meya
wa Ferraz de Vasconcelos, walipo ubuni mtandao
huo wa kijamii.
Mpaka sasa dos Santos amewekeza $16,000
katika uanzilishi wa mtandao huo.

No comments:

Post a Comment