Kuna mengi sana unaweza ukawa
ushasikia sana kuhusu njia nzuri za
kuchaji simu yako. Pia utakuwa
umeshasikia kuhusu ambayo hutakiwi
kufanya ukiwa unachaji simu.
Je yana ukweli wowote?
Leo tutakuelezea kwa uchache na kwa
ukweli mambo muhimu kuhusu kuchaji
kwa simu na usalama wa betri za simu
wakati tukiwa tunazichaji.
1. Kutumia chaja ambazo si za
makampuni ya simu zinaua simu
Hapana, hakuna ukweli kabisa katika hili
ila ukweli ni kwamba usitumie chaja za
ubora mbovu. Chaja feki si chaja zote
ambazo hazitengenezwi na kampuni
husika ya simu bali ni chaja ambazo zipo
chini ya kiwango. Na hizi utazigundua
kupitia bei zake, usikubali kumiliki simu
ya gharama halafu ukawa mbahili katika
kununua chaja za uhakika kisa bei zake.
2. Usitumie simu yako wakati unaichaji
Si kweli, ni kweli zamani sana, kwa sasa
teknolojia inayotumika kwenye chaja na
simu ni salama kabisa. Cha kuhakikisha
ni kwamba unatumia chaja zilizo na
kiwango/ubora wa uhakika (original/
quality). Kumbuka hapa haimanaanishi ni
kwamba lazima iwe ni yenye lebo/nembo
ya kampuni husika bali hili ni suala la
kuwa ni chaja yenye ubora wa uhakika.
3. Usizime simu yako kamwe!
Si kweli! Unashauliwa kuzima simu yake
angalau ata mara moja kwa wiki kwa
angalau lisaa. Simu kama vifaa vingine
vyote vya umeme ni muhimu kupata
muda wa kupumzishwa. Na jambo hili
ndio linaboresha zaidi uhai wa simu yako.
4. Kuchaji simu usiku kucha kutaiua/
haribu
Usikilize hii…si kweli! labda kama
unatumia simu iliyotengenezwa miaka ya
1980 :-). Teknolojia imekua sana, fahamu
ya kwamba simu zote za siku hizi
zitaacha kutumia umeme pale simu yako
itakapochaji hadi asilimia 100! Itaacha
kuchaji! Hakuna madhara! Ila hii
haimaanisha ndio uiache kwa zaidi ya
masaa 15!
5. Subiri hadi chaji iwe chini kabisa au
imeisha ndio uchaji
Hili sio kweli! Ukweli ni kwamba kuchaji
mara kwa mara ndio kunasaidia zaidi
kuongeza maisha ya betri yako. Kumbuka
kuchaji mara kwa mara si kila baada ya
dakika 5, bali ni kwamba usisubiri chaji
iwe chini ndio uchaji, na si lazima ukiweka
kwenye chaji usiitoe hadi imejaa.
6. Kuna aina kuu mbili za mabetri
yanatumika kwa sasa
Kuna mabetri yanayotumia teknolojia
ya Lithium-Ion (Li-ion) na Lithium-Ion-
Polymer (Li-ion polymer/Lithium
Polymer). Kuna teknolojia nyingi
zilizokuwepo zamani ila kwa sasa hizi
ndio zinazotumika zaidi. Na zinatumika
kutokana na ubora wake. Lithium-Ion (Li-
ion) zinatumika zaidi katika simu nyingi
zaidi wakati mabetri ya Lithium-Ion-
Polymer yanatumika zaidi katika laptop na
baadhi ya simu pia. Lithium-Ion-Polymer
ndio teknolojia bora zaidi na salama zaid,
lithium-Ion ni salama pia kwa kiwango
kikubwa sana ila lithium-ion-polymer ni
zenye ubora zaidi na hii inaweza kuwa ni
sababu kubwa zinatumika kwenye laptop
nyingi tayari. Teknolojia hizi zimefanya
ulipukaji ovyo wa mabetri ya simu kuwa
mgumu sana kuliko unavyofikiri.
Wednesday, July 8, 2015
Mambo 6 Yasiyo ya Kweli kuhusu Kuchaji Simu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment