Neno Android lina maana kadhaa, ila kimsingi, yote
yana maana nzuri na mwisho wa siku inaeleweka.
Neno Android linatumika sana kwenye intaneti, na
inaweza kutumika kumaanisha kitu flani wakati siyo
chenyewe na bado mtu akaeleweka. Android
inaweza kumaanisha mfumo wa vifaa vya kiganjani,
simu, laptopu, TV, na siku zinavyozidi kuenda,
karibu kila kitu, hata roboti.
Katika kujaribu kulielezea neno ‘Android’, waandishi
kama Jerry Hidenbrand wa AndroidCentral ,
wanaweza kumaanisha moja ya vitu vitatu:
‘The Open Android’ – Android Huria
Kampuni ya Google inaongoza utengenezaji wa programu-endeshaji huria (‘Open Source Operating System’)
iitwayo Android. Programu-endeshaji hii ina kila kitu cha msingi na hata zaidi vinavyohitajika kuwasha na
kutumia kifaa cha kielektroniki, na mtu au taasisi yoyote inaweza kuichukua na kuitumia itakavyo. Pamoja na
mfumo huo kuna viwezeshaji pia vya kumpa urahisi mtu yoyote mwenye nia kutengeneza programu za ziada
kwa urahisi, ambazo anataka zitumike kwenye kifaa chake.
Neno fasaha kwa Android hii ni The ‘Android Open Source Project’ (AOSP) na ndio kinachomaanishwa mtu
anaposema Android ni huru na bure. Ina wezekana umeshawahi kucheza na Android kama hii kama umewahi
ku-root na kuweka ROM yako kwenye kwenye simu yako. Watengenezaji wa ROM huchukua AOSP na
kuirekebisha kufaa simu au tabiti aina flani.
Android inayotumiwa na Watu wengi
Android iliyozoelewa na wengi huonekana kama
hivi.
Kwa watu wengi, Android wanayoitumia siyo AOSP.
Vitu kadhaa vinaweza kubadilishwa na kuongezwa
kutengeneza Android tofauti kabisa.
Iwe una simu ya Nexus au ya Samsung au ya
Motorola au simu nyingine yoyote inayoendeshwa
na Android, kila moja inatumia Android
iliyobadilshwa na kuongezewa mambo mambo flani
tofauti.
Utofauti wa Android kama hii si wa bure na hauwezi
kusambazwa kama unavyopenda kisheria ingawa
watu hufanya hivi na hamna anayesumbuliwa.
Utofauti unaokuja na Androidi hizi tofauti ndiyo
unaoweka ushindani kwa watengenezaji tofauti wa
Android. Watu wengine huchagua Samsung au HTC
au Sony au nyinginezo kutokana na vitu kila moja
ilivyonavyo.
Android Ulioshikilia Sasa
Kwa watu wengi, Android ni kitu chochote
kisichokuwa iPhone, Blackberry au Windows
Phone. Wao hawaji kuwa hii ni Samsung,
Huawei wala nini.
Kama wewe ni mtu unayefuatilia sana maswala ya
Teknolojia na hasa teknokona, tayari unajua
kwamba simu ulioshika ni ya aina gani – Samsung,
Tecno, Sony, Huawei, yoyote. Hatahivyo, kuna
watu, tena wengi ambao wao wanachojua ni
kwamba wana simu ya ‘Android’.
Kama vile Lumia 535 ni Wndows Phone, Blackberry
8900 ni Blackberry na iPhone 4S ni iPhone, Tecno
yako ni Android.
Kila Android ya kisasa inaweza kuendesha app
zilezile, kutumia huduma za Google vilevile na hata
kuunganisha watu kihisia sawia. Android tofauti
zimetengenezwa kitofauti ila usawia unabaki
palepale.
Kwahiyo, Android ni Nini Hasa?
Tumeeleza vitu vitatu vinavyoweza kumaanisha Android. Google wanatumia neno Android kumaanisha vitu
viwili tofauti (na sisi watumiaji tunafanya hivyo) kwa sababu, mara nyingi inaeleweka wanachomaanisha!
Ukweli ni kwamba, ukimaansha Android kama AOSP, au kama simu yako ya Samsung au kama kuitofautisha
simu yako na iPhone wakati wa mabishano ya ipi zaidi, Android ni Android – hata kama imewekewa manjonjo
kadhaa kuifanya ionekana kidogo tofauti na Android nyingine.
Chukulia mjadala huu kama hivi:
1. Ukiona mfanyakazi wa Google akiandika kitu
kama hiki mtandaoni:
“mkdir android ;
cd android ;
repo init -u git://android.git.kernel.org/platform/
manifest.git ;
repo sync ;
make”
mtu huyu anamaanisha moja ya maana ya Android
2. Ukisikia au kuona kampuni ya Google au kampuni
ya Sony, Samsung au HTC ikitangaza simu yao
mpya ya Android, wanamaanisha Android nyingine:
ya kwao!
3. Ukisikia rafiki yako kanunua simu mpya ya
Android kutoka duka la simu, hiyo ni maana
nyingine ya Android!.
Sunday, August 16, 2015
SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Android ni nini haswa?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment