Leo mida ya saa nane ama tisa mchana mitaa fulani ya Kariakoo kulikuwa na ukamatajwi wa utapeli uliofanywa na mbibi ambaye anafanya biashara ya kuuza mayai ya kienyeji kwa kutembeza mitaani ikiwa mayai yenyewe ni mabovu.
Mbibi huyo hakuweza kufahamika kwa majina yake kwa haraka wala mbaba huyo pia.
Mbaba ambaye alimfuma mbibi huyo katika duka moja Kariakoo wakati huyo mbaba ananunua mzigo ghafla bin vuu akamuona mbibi aliyemtapeli tangu miezi kadhaa mwaka huu 2015.
Tukio lilikuwa hivi:
Mbaba: Habari yako mama?
Mbibi: Nzuri.
Mbaba: Nahitaji kunununa mayai.
Mbaba: Sawa. (Akatua mzigo wake wa ndoo yake yenye mayai).
Mbaba: (Akamuuliza mbibi). Unanikumbuka lakini?
Mbibi: Hapana sikukumbuki.
Mbaba: (Akajieleza namna alivyokutana naye). Uliniuzia mayai mabovu miezi kadhaa iliyopita maeneo ya ofisini kwangu n.k.
Mbibi: Hapana sio mimi.
Mbaba: (Akatoa simu akampigia mtu ambaye wakati anauziwa mayai alikuwepo aje pale eneo la tukio...mtu huyu ni mfanyakazi wake.-Hallo! Sasa yule mbibi aliyeniuzia mayai mabovu nimemkamata uje sasa tumpeleke polisi.
(wakawa wanamsubiri).
Mbibi: (Akajikaza kwa kusema).-Twende mimi siogopi twende tu.)
Muda kidogo mbibi yule akaomba aende chooni akajisaidie ila mbaba na watu wa pale wakamkatalia baada ya kulalamikiwa sana na watu labda kweli.
Mbaba: (Akatoa wazo kabla ya kwenda polisi wayavunje mayai na kama kuna mazima atayalipa na kama kuna mengi mabovu kuliko mazima atampeleka polisi.)
Kulikuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu ambapo wahisi kama anasingiziwa yule mbibi.
Yule mbaba akatoa hela ya kununua chombo cha kupasulia mayai ila kuna mtu alijitolea chombo hiko na baadae yule mfanyakazi alifika na ndiye aliyekuwa mvunjaji wa mayai.
Kabla ya kuja yule mfanyakazi...mbibi alioneshwa namba na yule mbaba ambayo mbibi alimpa wakati ule anamuuzia mayai na alimuonesha kama ushahidi na mbibi alidhibitisha kama ni kweli yake ila aliibiwa simu na hivyo ilikuwa haipatikaniki.
Baada ya kuja mfanyakazi na kuvunja mayai kuanzia yai la kwanza mpaka la sita yalikuwa mabovu. Hivyo watu wakajua ni kweli huyo mbibi ni TAPELI.
Mbibi huyo alikubali kwenda polisi maana alishafumaniwa kwamba biashara yake si halali. Alipoenda polisi alishtakiwa na kutoa kiasi cha Tsh. 40,000/= kumpatia mbaba yule. Ila haikujulikana kama ni ya manunuzi ya yale mayai ndio yalivyouzwa ama nusu hasara au la kwa vile tangu mwanzo hatukuweza kupata taarifa kamili kama ni kiasi gani alichouziwa yale mayai.
No comments:
Post a Comment