Mchezaji mpya wa Chelsea Pedro Rodriguez
ameanza maisha mapya ndani ya klabu yake mpya
baada ya kuifungia bao moja huku akitoa pasi ya
mwisho kwa bao lingine katika mchezo wa ligi kuu
ya England ambao Chelsea ilishinda kwa matokeo
ya 3-0.
Pedro alisajiliwa na Chelsea katikati ya wiki iliyopita
alifunga moja kati ya mabao matatu ambayo
yalifungwa na wachezaji raia wa Hispania ndani ya
Chelsea ikiwa ni ishara ya matunda ya usajili
ambao Chelsea imeufanya .
Ushindi huu dhidi ya Westbromwich Albion
unakuwa ushindi wa kwanza kwa Chelsea msimu
huu baada ya timu hii kuanza ligi kwa kasi ya chini
ambapo walifungwa na Manchester City huku
wakitoka sare kwenye mchezo wao wa kwanza
dhidi ya Swansea .
Sunday, August 23, 2015
MICHEZO: Pedro makali yangu yaleyale ya Barcelona
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment